vid

Kingwendu na video Tz, mixing za Producer One na Christian Bella na video ya ‘Nashindwa’…#255

87da6f743f0cb8df9a7ee5bb86579024Mchekeshaji Kingwendu amesema wasanii waotaka kumshirikisha kwenye video au movie,  kitu cha kwanza kuangalia ni ujumbe na kama msanii huyo anajulikana endapo hajulikani gharama zake zinaanzia milioni moja hadi laki tano ila kwa msanii mkubwa huwa anafanya laki mbili au tatu kwasababu anajua kuna siku na yeye atamhitaji kwenye kazi zake..
DSC04474Producer One ambae amehusika kufanya mixing ya wimbo mpya wa Chid Benz  amesema, ameanza kufanya production muda mrefu lakini hakutaka kufanya rasmi kutokana kushindwa kufanya majukumu mengine, lakini kwasasa atakuwa anafanya production kama alivyofanya kwenye Album za wasanii mbalimbali.
bellMsanii wa mziki wa dance nchini Christian Bella amesema video ya wimbo wake mpya wa ‘Nashindwa’ ndio video aliyofanya kwa gharama kubwa toka aanze mziki, video ambayo imefanywa na director mkali Bongo Adam Juma ambayo ameifanyia nchini Afrika Kusini.
Kusilikiza story zote za 255 bonyeza play hapa chini...

____________________________________________________________________________________________

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni