
Unadhani iko hiyo pekeake?? Bella amesema ziko nyingi ambazo anazipenda pia.

Christian Bella
Bella amesema kwa upande wa nyimbo za nje ya TZ anatamani kuurudia wimbo wa Chris Brown ‘With You’ .. kwa sasa anafanya project ya kurudia nyimbo 10 za Bongo Fleva, iliwemo Uhali Gani -Q Chief, ‘Me&U’ -Ommy Dimpoz, feat. Vee Money, ‘Awena’ -Kassim Mganga na TID –Asha.
Msanii Kassim Mganga amesema hakuogopeshwa na maneno yaliyokuwa yanahusisha ishu ya msanii kuoa na kufeli kimuziki.. kwa upande wake anasema mke lazima awe rafiki kwa muda mrefu kabla ya kuoana ili wapate muda wa kujuana na kuheshimiana.
Kassim anaamini hakuna mafanikio ya mwanaume bila mwanamke, ishu ya kufanikwa au kushuka kwenye muziki ni mtu mwenyewe.
Info ya mwisho amesikika star Ali Kiba ambae ametangaza rasmi kuacha kufanya muziki wa playback, kuanzia sasa burudani ya show yoyote ya Kiba itakuwa ni Live Band.. amesema kajipanga kwa hilo, tayari ana vifaa vyake.
Kashea na sisi hiki kingine kipya, amesema kumbe muziki wa live band inamfanya msanii awe serious.
Kusikiliza stori zote za 255 bonyeza play hapa chini mtu wangu…_________________________________________________________________________________________
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni