vid

Justin Bieber Matatani.

Teen Choice Awards 2012 - Show

Siku zote kwenye mapenzi wivu haukosekani , hilo limedhihirika hivi karibuni ambapo rapa Big Sean alidhihirisha hisia za wivu kumuelekea mpenzi wake Ariana Grande baada ya mwanamuziki huyo nyota wa miondoko ya Pop kuonekana kama ‘anabambiwa’ na mwanamuziki mwingine Justin Bieber wakati wawili hao wakiwa ‘wanaperfom’ jukwaani.
Bieber alionekana kuvuka mipaka kwa jinsi alivyokuwa akimshika Ariana Grande kitendo ambacho Big Sean hakukifurahia hata kidogo.

Rapa huyo toka Detroit alikimbilia kwenye twitter ambako alieleza hisia zake na kuonyesha jinsi alivyokerwa na kitendo hiki .
Justin Bieber 'akimbambia' Ariana Grande wakati wakiwa jukwaani.
Justin Bieber ‘akimbambia’ Ariana Grande wakati wakiwa jukwaani.
Big Sean aliandika kwenye Twitter kuwa ‘Huyu Kijana anakaribia kufundishwa somo la kuacha kumshika msichana wangu namna hii’ Tweet ambayo ilitasiriwa kama hisia za wivu toka kwa Big Sean.
Tweet ambayo Big Sean aliituma baada ya kuona picha ya Mpenzi wake Ariana Grande na Justin Bieber jukwaani.
Tweet ambayo Big Sean aliituma baada ya kuona picha ya Mpenzi wake Ariana Grande na Justin Bieber jukwaani.
Ariana Grande kwa upande wake hakuonyesha kuridhishwa na jinsi ambavyo Bieber alikuwa anamshikashika na alionekana akiwa anamkwepa mara zote wakiwa jukwaai .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni